Tuesday, January 2, 2018

VITA VYA KIROHO

Napenda nikutakie amani ndugu shalom:Napenda nishirikiane nawe kuhusu vita vya kiroho kumbuka tunaishi katika ulimwengu unaoonekan pia upo ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama twaweza kusema ulimwengu wa giza au wa nuru kwa ujumla twasema ulimwengu wa roho.Tunaposema vita vya kiroho maana yake ni ushindani kati ya majeshi upande wa shetani na upande wa Mungu lengo kuu la ibilisi katika vita hivyo ni kuhakikisha watu hawamuamini yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa msisha yao na wale walioamini wakate tamaa na kurudi nyuma yaani kuiacha njia ya wokovu,kuleta magonjwa huzuni,ugomvi na vifungo mbalimbali Namna ya kushinda hiyo vita ni kuvaa silaha zote za Mungu.                  WAEFESO 6:10-20.Na wala sio kuvaa silaha moja ni zote  na ukipungukiwa na silaha moja tu kushindwa ni rahisi ndo mana tukaambiwa tuvae silaha zote wengi hushindwa katika vita vya rohoni sababu hushindwa kuvaa silaha zote maana ukipungukiwa silaha moja mfano mfano kuvaa dirii ya haki kifuani adui atapiga hapo hapo ambapo hamna hiyo silaha.Daudi alimpiga goliathi na jiwe kwenye paji ya kichwa chake sababu ndipo palikuwa na uwazi hivyo katika safari yako ya kwenda mbinguni usiache nafasi yoyote ambayo adui yako aweza kukuonea.Tuvae silaha zote pasipo sahau au kuacha yoyote.ubarikiwe ushindi ni wako.
Na Agnes mwasambili
0769519697

No comments:

Post a Comment