Thursday, January 11, 2018

MADHARA YA DHAMBI

Ndugu napenda kukusalimu katika jina la Yesu,uliyedhaifu Bwana akuponye sasa uliyedhaifu akuhuwishe sasa.Naomba nikushirikishe madhara ya Dhambi,1 Yohana 3:4, Neno linasema dhambi ni uasi , hakuna dhambi ndogo wala kubwa mbele za Mungu na hukumu za dhambi zote zafanana ni kutupwa motoni tena ni milele.
             MADHARA YA DHAMBI.
1.Unapotenda dhambi unajiondoa katika nafasi aliyokuweka Mungu na kujitengenezea nafasi yako.Mwanzo 3:9 kwa mfano kiuchumi ilibidi use hatua Fulani waweza ondolewa sababu
 ya kukosa uaminifu katika biashara yako au ndoa yako ukaishi katika mashaka na hofu.Mwanzo 4:16 kaini alitoka katika USO Wa Bwana aliondolewa katika nafasi ya kwanza.

2.Unaishi kwa hofu.Mwanzo 32:9-12. Yakobo alimuogopa Esau ndugu yake sababu alimchukulia mubaraka wake wa mzaliwa wa kwanza hivyo alihisi Esau atalipiza kisasi kwake hila aliyoifanya Yakobo ilisababisha awe na hofu.

 3.Dhambi Ina kisasi unapotenda lolote la uovu au baya jua malipo yapo tu.Mwanzo 4:24.

 4.Dhambi uleta mauti ya kiroho na kimwili.

Ubarikiwe.
Na Agnes mwasambili
0769519697.

No comments:

Post a Comment