Kuomba sawasawa na mapenzi ya MUNGU maana yake ni kuomba sawasawa na matakwa ya MUNGU.Kumbe katika kila maombi yako ni vyema kwanza kutafuta matakwa ya MUNGU juu ya hayo unayoyaombea.
Kwa njia hiyo tunagundua kwamba kuna makundi mengi ya maombi yakiwemo:
1. Maombi sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
2. Maombi sawasawa na mapenzi ya muombaji.
3. Maombi sawasawa na mapenzi ya muombaji ila ndani yake kuna mapenzi sawasawa na kusudi la MUNGU.
Lakini muhimu kujua ni kwamba tukiomba sawasawa na mapenzi yake MUNGU yeye hutusikia na kutujibu.
Tujajifunza nini?
Kumbe katika baadhi ya maombi unayoomba ndani yake kuna mapenzi ya MUNGU hivyo kabla hujaomba taka/tafuta kwanza kujua nini mapenzi ya MUNGU kwa hayo unayotaka kuombea.
Mfano kijana anaweza kuomba apewe mke kumbe mapenzi ya MUNGU sio tu kumleta huyo mke Bali kwanza huyo anayetaka kupewa mke anatakiwa labda afunguliwe kwanza yeye ili aweze kuhimili ndoa.
Lakini ninachojua Mimi ni kwamba ROHO MTAKATIFU akikuongoza kuomba hakika hapo moja kwa moja unakuwa unaomba sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
Kumbuka ROHO MTAKATIFU hutuombea Biblia ndivyo inavyosema lakini maombi hayo ya ROHO MTAKATIFU ni kupitia vivywa vyetu na hutuombea kupitia maombi yetu kwa kutuelekeza kuliendea hitaji sahihi.
Tukumbuke na hii kwamba tukiomba tu sawasawa na mapenzi yetu au tamaa zetu kupokea ni ngumu.
Yakobo 4:3 "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu."
MUNGU akubariki sana

No comments:
Post a Comment