Tuesday, April 25, 2017

USHIRIKA MTAKATIFU


Ushirika ni neno linalotokana na kushirikiana.
Tulipompokea YESU tulizaliwa katika familia ya MUNGU hivyo ni lazima tuwe na ushirika na wakristo wenzetu waliompokea YESU.
Yohana 1:12-13 Biblia inasema " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. "

Waliookoka wote ni familia ya MUNGU hivyo wanatakiwa kuwa na ushirika kama familia moja ya MUNGU.
Tunaitwa watoto wa MUNGU kwa sababu tuna ushirika na MUNGU.
Ndugu, naomba ujue kwamba ukipoteza ushirika na MUNGU unakuwa nje na ufalme wake.

Tu viungo katika mwili mmoja.
Tu askari katika jeshi moja.
Tu wenye uraia katika taifa moja liitwalo wateule wa KRISTO.
Sisi ni ushirika(2 Kor 12:14-27)
Tuna ushirika na MUNGU.
Tuna ushirika na BWANA YESU aliyetuokoa.
Tuna ushirika na ROHO MTAKATIFU anayetuongoza na kutufundisha.
Tuna ushirika sisi kwa sisi kama timu moja yenye malengo mamoja yaitwayo uzima wa milele.
Ushirika wetu unahusisha kukutana ibadani ili kujifunza neno La MUNGU pamoja.
Kuonyana ili asitokee wa kutoka nje ya mstari wetu uitwao wokovu wa KRISTO.
Nk.
Nawapenda wateule wote haijalishi wanatoka kanisa gani.
Wote ni watoto wa MUNGU kama wanaliishi neno La MUNGU.
Biblia inasema hivi.
MUNGU mmoja.
Imani moja.
Ubatizo mmoja.
BWANA mmoja.

No comments:

Post a Comment