Saturday, January 13, 2018

THAMANI IDUMUYO: MADHARA YA DHAMBI

THAMANI IDUMUYO: MADHARA YA DHAMBI: Ndugu napenda kukusalimu katika jina la Yesu,uliyedhaifu Bwana akuponye sasa uliyedhaifu akuhuwishe sasa.Naomba nikushirikishe madhara ya Dh...

Thursday, January 11, 2018

MADHARA YA DHAMBI

Ndugu napenda kukusalimu katika jina la Yesu,uliyedhaifu Bwana akuponye sasa uliyedhaifu akuhuwishe sasa.Naomba nikushirikishe madhara ya Dhambi,1 Yohana 3:4, Neno linasema dhambi ni uasi , hakuna dhambi ndogo wala kubwa mbele za Mungu na hukumu za dhambi zote zafanana ni kutupwa motoni tena ni milele.
             MADHARA YA DHAMBI.
1.Unapotenda dhambi unajiondoa katika nafasi aliyokuweka Mungu na kujitengenezea nafasi yako.Mwanzo 3:9 kwa mfano kiuchumi ilibidi use hatua Fulani waweza ondolewa sababu
 ya kukosa uaminifu katika biashara yako au ndoa yako ukaishi katika mashaka na hofu.Mwanzo 4:16 kaini alitoka katika USO Wa Bwana aliondolewa katika nafasi ya kwanza.

2.Unaishi kwa hofu.Mwanzo 32:9-12. Yakobo alimuogopa Esau ndugu yake sababu alimchukulia mubaraka wake wa mzaliwa wa kwanza hivyo alihisi Esau atalipiza kisasi kwake hila aliyoifanya Yakobo ilisababisha awe na hofu.

 3.Dhambi Ina kisasi unapotenda lolote la uovu au baya jua malipo yapo tu.Mwanzo 4:24.

 4.Dhambi uleta mauti ya kiroho na kimwili.

Ubarikiwe.
Na Agnes mwasambili
0769519697.

Tuesday, January 2, 2018

VITA VYA KIROHO

Napenda nikutakie amani ndugu shalom:Napenda nishirikiane nawe kuhusu vita vya kiroho kumbuka tunaishi katika ulimwengu unaoonekan pia upo ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama twaweza kusema ulimwengu wa giza au wa nuru kwa ujumla twasema ulimwengu wa roho.Tunaposema vita vya kiroho maana yake ni ushindani kati ya majeshi upande wa shetani na upande wa Mungu lengo kuu la ibilisi katika vita hivyo ni kuhakikisha watu hawamuamini yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa msisha yao na wale walioamini wakate tamaa na kurudi nyuma yaani kuiacha njia ya wokovu,kuleta magonjwa huzuni,ugomvi na vifungo mbalimbali Namna ya kushinda hiyo vita ni kuvaa silaha zote za Mungu.                  WAEFESO 6:10-20.Na wala sio kuvaa silaha moja ni zote  na ukipungukiwa na silaha moja tu kushindwa ni rahisi ndo mana tukaambiwa tuvae silaha zote wengi hushindwa katika vita vya rohoni sababu hushindwa kuvaa silaha zote maana ukipungukiwa silaha moja mfano mfano kuvaa dirii ya haki kifuani adui atapiga hapo hapo ambapo hamna hiyo silaha.Daudi alimpiga goliathi na jiwe kwenye paji ya kichwa chake sababu ndipo palikuwa na uwazi hivyo katika safari yako ya kwenda mbinguni usiache nafasi yoyote ambayo adui yako aweza kukuonea.Tuvae silaha zote pasipo sahau au kuacha yoyote.ubarikiwe ushindi ni wako.
Na Agnes mwasambili
0769519697

Monday, January 1, 2018

Mwaka mpya

Ndugu tunapoanza mwaka tafuta Kauli mbiu au neno la ushuhuda na ujasiri litakalo kupa nguvu unapoendelea katika siku za mwaka mimi nakuambia neno hili mwaka 2018 uwe mwaka wa kupokea na kuongezeka kwako kiroho,kiuchumi,kimwili na katika khali zote.Ubarikiwe.
Na Agnes mwasambili
0769519697.