Saturday, December 30, 2017

NYAKATI.

Ndugu napenda kukusalimu katika jina la Yesu kristo matumaini yangu u mzima wa afya uliye dhaifu pokea uponyaji sasa.Napenda nikushirikishe ujumbe huu kwamba:
Katika nyakati zote Mungu ni mwaminifu na hawezi muacha mwenye haki wake yawezekana ulipokuwa katika wakati wa furaha,amani, kicheko au mafanikio makubwa ndipo ulihisi Mungu anakupenda ukaona Mungu yupo pamoja nawe,ngoja nikukumbushe kwamba katika hali zote Mungu yupo katika huzuni,upweke,kilio au maumivu makali Yesu yupo nawe hisi uwepo wake elewa anakupenda tena anakuwazia mema jipe moyo songa mbele usiogope,ubarikiwe.
Zaburi 34:17-19.
Na Agnes Mwasambili
0769519697.

Saturday, July 22, 2017

Rafiki

Mwanadamu anatabia ya kubadilika waweza kuwa na rafiki akakusema vibaya,akakusengenya,akakusaliti au akakukataa au kukukana ndugu yawezekana mme,mke,mchumba,wazazi,watoto,ndugu au rafiki wamekuacha au kukusaliti elewa yupo rafiki wa kweli ambaye hajutii urafiki wenu ni mwaminifu mfariji wa kweli anakuwaazia mema hata kama wote watakuacha usiogope hawezi kukuacha kamwe shikamana naye,zungumza naye mshirikishe yale magumu unayopitia yupo tayari kukusaidia rafiki wa kweli ni YESU
Yohana 15:15
Na Agnes Mwasambili
0769519697

Friday, July 21, 2017

THAMANI IDUMUYO: Thamani idumuyo

THAMANI IDUMUYO: Thamani idumuyo: Ndugu katika Kristo usikubali kumuacha Yesu sababu ya chochote au jambo lolote ila acha vyote kwa ajiri ya uzuri wa Kristo.Yawezekana kwako kazi,Mali, pesa ,dhahabu, Mke, Mme,Watoto,shamba,mpenzi,elimu vinathamani kwako tambua Ipo Thamani isiyo haribika nayo ni Yesu au wokovu.Yesu ni thamani idumuyo.Ubarikiwe
Na Agnes Mwasambili
0769519697.

Tuesday, April 25, 2017

USHIRIKA MTAKATIFU


Ushirika ni neno linalotokana na kushirikiana.
Tulipompokea YESU tulizaliwa katika familia ya MUNGU hivyo ni lazima tuwe na ushirika na wakristo wenzetu waliompokea YESU.
Yohana 1:12-13 Biblia inasema " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. "

Waliookoka wote ni familia ya MUNGU hivyo wanatakiwa kuwa na ushirika kama familia moja ya MUNGU.
Tunaitwa watoto wa MUNGU kwa sababu tuna ushirika na MUNGU.
Ndugu, naomba ujue kwamba ukipoteza ushirika na MUNGU unakuwa nje na ufalme wake.

Tu viungo katika mwili mmoja.
Tu askari katika jeshi moja.
Tu wenye uraia katika taifa moja liitwalo wateule wa KRISTO.
Sisi ni ushirika(2 Kor 12:14-27)
Tuna ushirika na MUNGU.
Tuna ushirika na BWANA YESU aliyetuokoa.
Tuna ushirika na ROHO MTAKATIFU anayetuongoza na kutufundisha.
Tuna ushirika sisi kwa sisi kama timu moja yenye malengo mamoja yaitwayo uzima wa milele.
Ushirika wetu unahusisha kukutana ibadani ili kujifunza neno La MUNGU pamoja.
Kuonyana ili asitokee wa kutoka nje ya mstari wetu uitwao wokovu wa KRISTO.
Nk.
Nawapenda wateule wote haijalishi wanatoka kanisa gani.
Wote ni watoto wa MUNGU kama wanaliishi neno La MUNGU.
Biblia inasema hivi.
MUNGU mmoja.
Imani moja.
Ubatizo mmoja.
BWANA mmoja.

Sio makanisa yote hutumia Biblia kama ndio kanuni yao ya imani.


Sio makanisa yote hutumia Biblia kama ndio kanuni yao ya imani.
Sio wote wanaoitwa wakristo wanaye KRISTO ndani yao.
Sio kila anayesema BWANA YESU asifiwe yuko safari ya mbinguni.
Kuokoka ni kujikana sio kufuata dini ya wazazi ambayo dini hiyo haijawahi kuwasaidia wazazi wako maana dhambi bado zimewakamata hata kama wana zaidi ya miaka 40 tangu waanze kuhudhuria kwenye dini.
Aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja na kahaba.
Jiulize swali hili;
Kama kuna watu wanasujudia sanamu wakati Biblia inakataza, Hata kama wanaitwa wakristo je wanajitambua na wanamtambua BWANA YESU?
biblia inasema " Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale
wawili watakuwa mwili mmoja. ” 1 Wakorintho
6:16.
Kama kuna watu ni mwili mmoja na kahaba Je unadhani walio mwili mmoja na sanamu watakosekana?
Kama watu ni mwili mmoja na kahaba je walio mwili mmoja na shetani watakosekana?
Unaloga na kanisani unaenda wewe ni mwili mmoja na shetani.
Unaiba na kanisani unaenda wewe ni mwili mmoja na shetani.
Sio wote waitao BWANA BWANA watakaoingia paradiso Bali watakatifu tu.

MAOMBI SAHIHI NI YAPI?



1. Maombi sahihi ni maombi kwa MUNGU yanayoambatana na utakatifu.

2. Maombi sahihi ni maombi kwa MUNGU kupitia jina la YESU KRISTO.

3. Maombi sahihi ni maombi ya Imani katika jina la YESU KRISTO

4. Maombi sahihi ni maombi katika ROHO MTAKATIFU.

5. Maombi sahihi ni maombi sawa sawa na mapenzi ya MUNGU.


NENO LA LEO

1 Yohana 5:14 “ Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,atusikia’.
Kuomba sawasawa na mapenzi ya MUNGU maana yake ni kuomba sawasawa na matakwa ya MUNGU.
Kumbe katika kila maombi yako ni vyema kwanza kutafuta matakwa ya MUNGU juu ya hayo unayoyaombea.

Kwa njia hiyo tunagundua kwamba kuna makundi mengi ya maombi yakiwemo:
1. Maombi sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
2. Maombi sawasawa na mapenzi ya muombaji.
3. Maombi sawasawa na mapenzi ya muombaji ila ndani yake kuna mapenzi sawasawa na kusudi la MUNGU.
Lakini muhimu kujua ni kwamba tukiomba sawasawa na mapenzi yake MUNGU yeye hutusikia na kutujibu.
Tujajifunza nini?
Kumbe katika baadhi ya maombi unayoomba ndani yake kuna mapenzi ya MUNGU hivyo kabla hujaomba taka/tafuta kwanza kujua nini mapenzi ya MUNGU kwa hayo unayotaka kuombea.

Mfano kijana anaweza kuomba apewe mke kumbe mapenzi ya MUNGU sio tu kumleta huyo mke Bali kwanza huyo anayetaka kupewa mke anatakiwa labda afunguliwe kwanza yeye ili aweze kuhimili ndoa.
Lakini ninachojua Mimi ni kwamba ROHO MTAKATIFU akikuongoza kuomba hakika hapo moja kwa moja unakuwa unaomba sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
Kumbuka ROHO MTAKATIFU hutuombea Biblia ndivyo inavyosema lakini maombi hayo ya ROHO MTAKATIFU ni kupitia vivywa vyetu na hutuombea kupitia maombi yetu kwa kutuelekeza kuliendea hitaji sahihi.

Tukumbuke na hii kwamba tukiomba tu sawasawa na mapenzi yetu au tamaa zetu kupokea ni ngumu.
Yakobo 4:3 "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu."
MUNGU akubariki sana

NDOA NI NINI


Ndoa ni makubaliano kati ya mwanaume asiye na mke na mwanamke asiye na mume kwa ajili ya kuishi pamoja kama mke na mume.
Makubaliano hayo ni lazima yathibitishwe na wazazi wa pande zote mbili na serikali na Kanisa la MUNGU.

Kwanini wazazi wahusike?
Ni kwa sababu ni wazazi.
Kwanini serikali?
Ni kwasababu ni mamlaka inayoweza kumsaidia mwanandoa kupata haki zake hata kipindi mwenzi wake hayupo.
Uhusika wa serikali ni kutoa vyeti vya ndoa.
Mfano mume akifariki kisha ndugu wa mume wanamfukuza mjane na kumnyang'anya Mali, akishitaki serikalini cheti cha ndoa kitahitajika ili kumthibitisha kwamba alikuwa mke halali wa yule mwanaume.
Ndio maana serikali hutoa vyeti viwili yaani anayeolewa anapewa na anaoa anapewa.
Hata hivyo vyeti vya ndoa vina kazi nyingi pia.

Kwanini kanisa la MUNGU?
Ni kwa sababu lazima tuyafanyayo yafanyike katika Bwana YESU.
Kumbuka na sisi tu wa YESU.
Na MUNGU ndio mwanzilishi wa ndoa.
Na ndoa inahitaji ulinzi wa MUNGU na utakatifu.
Kuna mengi sana katika hilo la kwanini ni muhimu kumhusisha MUNGU kwenye ndoa.
Biblia inasema

Wakolosai 3:17 "Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye."

Baadhi ya maswali na majibu kuhusu ndoa


Baadhi ya maswali na majibu kuhusu ndoa niliyoulizwa na rafiki yangu mmoja.
Unaweza kujifunza kitu pia.
Karibu.

Kwa kuwa NDOA NI AGENDA YA KIROHO KABISA...
JE, ...
1. maandiko yanasemaje juu ya *UKOMAVU WA MTU KIROHO*? kabla ya kuingia kwenye ndoa
--ili aweze kuzaa matunda mema ya rohoni!!

2. Mtu atajuaje kuwa kwa sasa amekomaa vya kutosha KUINGIA *ndoani* ?
3. Vijana wengi wanahudhuria kwenye SEMINA NYINGI ZA NDOA ,,lakini bado wakiingia *ndoani* ni *MGOGORO* tu.
Nini *SHIDA kuu HAPA*?
-------
nawasilisha...


Majibu yangu.

Swali la kwanza ulilouliza.
Maandiko yanasemaje juu ya ukomavu wa kiroho kabla ya kuingia kwenye ndoa?
Majibu yangu ni haya.

1. Hatukui kiroho ili tuingie kwenye ndoa Bali inatupasa kukua kiroho ili tumpendeze MUNGU na itusaidie kushinda maovu ya dunia na kila kilicho kinyume na MUNGU.
Kwenye ndoa hakuhitaji sana kukua kiroho Bali kunajitaji kukua kiufahamu juu ya Masuala ya ndoa.
Biblia inamtaka kila mwamini kukua kiroho maana ni kwa faida yake katika maisha ya kiroho na sio maisha ya ndoa tu.
Ila kukua kiroho kunaweza kumsaidia mtu kuimudu vyema ndoa yake.
Ila pia kuna watu wamekua sana kiroho lakini ndoa zao zina matatizo makubwa kwa sababu tu kukua tu kiroho hakumfanyi mtu awe na ndoa njema.
Kukua kiroho ni kuukulia Wokovu.
1 Petro2:2 ''Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;''

Swali la Pili
Mtu atajuaje kuwa sasa amekomaa vya kutosha ili kuingia katika ndoa?
Majibu yangu.
Suala la mtu kujua kwamba amekomaa na anaweza sasa kufunga ndoa ni suala ni mtu binafsi mhusika ila tu asiwe mtoto maana watoto hawaruhusiwi kuoa wala kuolewa.
Kuna wengine hujua wamekomaa na kuanza kutafuta wachumba ili wafunge ndoa wakiwa na miaka 20.
Kuna wengine huwa hawajitambui kama wamekomaa na wanatakuwa kufunga ndoa hata wakiwa na miaka 35 au 49, hao hadi washtuliwe na watu wa karibu yao.
Kuna wengine hujigundua kwamba sasa wamekomaa na wako tayari kufunga ndoa wakiwa na miaka 30 au wengine 45.
Ndio maana nimesema kwamba umri wa mtu kujijua kwamba anatakiwa kuoa au kuolewa ni juu ya ufahamu wa mhusika.

Biblia kwa andiko fupi na lililokamilika inasema.
"Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.-1 Kor 7:9
Mtu ana miaka kuanzia 24 hadi 50 na hajaoa na ni mzima nadhani yampasa kuoa maana atawaka tamaa sana na tamaa hizo asipojua kumcha MUNGU inaweza kuwa hatari kwake.
Tukumbuke pia wanawake wana ukomo wa umri katika kuzaa hivyo kama mwanamke ana miaka 55 na hataki kuolewa huku akitamani siku moja kuolewa na kuzaa watoto nadhani inaweza kumsumbua baadae kama muda wa kuzaa utakoma.

Swali la tatu.
Vijana wengi wanahudhuria semina za ndoa lakini bado wakiingia kwenye ndoa ni migogoro tu.
Tatizo ni nini?

Majibu yangu ni haya.
Migogoro katika ndoa hutokana na mambo mengi na mengine inawezekana hata kwenye semina za ndoa hawakufundishwa.
Ona haya.
1. Kwenye semina za ndoa mtu anaweza kufundishwa jinsi vya kukaa na mwenzi wake lakini asifundishwe kwamba muujiza uliopatikana kwa maombi hutunzwa kwa maombi.
Hivyo wengine wakiingia kwenye ndoa maombi hukoma na kufunga kunafutika na kwa njia hiyo shetani anapanda magugu na kuiathiri ndoa.

2. Kwenye semina za ndoa mnaweza kufundishwa jinsi ya kuandaana na kuambiana maneno matamu, lakini msifundishwe kibiblia jinsi ya kila mwanandoa kukaa kwenye nafasi yake kiroho na kimwili katika ndoa.
3. Semina za ndoa zinaweza kufundisha usafi wa mazingira na miili lakini usifundishwe jinsi ya kuishinda tamaa
Nyongeza A ni hii.
Kuna semina nyingi sana za ndoa lakini Mimi nawashauri watu kuhudhuria semina za ndoa ambazo walimu ni watumishi wa MUNGU waliookoka, maana hao watafundisha Semina Kibiblia na sio kijinsia na kimtazamo.

Ziada B ni hii.
Vyanzo vya ndoa kuwa na migogoro.
1. Kukosa maombi ya kina.
2. Kumruhusu shetani kuwatawala.
3. Kutokukaa kila mtu katika nafasi yake.
4. Kutokumcha MUNGU.
5. Msingi mbovu wa ndoa
6. Kufanyia kazi maneno


ya watu wabaya.
7. Kutojua jinsi ya kuufanya upya upendo uliopoa.

Nyongeza C ni hii.
Neno la MUNGU limekamilika hivyo kuhudhuria semina za neno la MUNGU, mikutano ya injili na kuhudhuria ibada na maombi kuna msaada zaidi huko kuliko hata semina za ndoa.
Ubarikiwe sana.
By Mwinjilisti Peter Mabula
Mabula1986@gmail.com.
0786719090
0714252292

BAADA YA YESU KRISTO KUFA MSALABANI HAYA YALITOKEA.



Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Mathayo 27:51-54 '' Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda YESU, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa MUNGU.''

1. Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kutoka juu hadi chini.
Kwanini ilikuwa hivyo?
YESU alifanya hayo ili Katika maombi yetu na kukubaliwa kwetu na MUNGU basi tuwe sawa wote tuliookolewa na yeye YESU KRISTO.
Kwa njia hiyo MUNGU aliondoa tofauti ya patakatifu na patakatifu pa patakatifu ili kila Mteule awe na kibali cha kupaingia patakatifu pa patakatifu kwa njia ya maombi.
Kumbuka Mwanzo waliokuwa wanaruhusiwa kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni mtu mmoja tu yaani kuhani mkuu, na yeye aliingia mara moja kwa mwaka.
Kwa Njia ya YESU KRISTO kila mwamini sana anaweza akaingia patakatifu pa patakatifu na kujibiwa hitaji lake na MUNGU.

Biblia inajibu juu ya hilo, Waebrania 9:8-12 ''ROHO MTAKATIFU akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama; ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye, kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya. Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. ''

Maana yake kila mtu sasa katika KRISTO YESU anaweza kumwendea MUNGU Baba kwa njia ya maombi na kukubariwa, sio lazima awe kuhani au mchungaji au askofu bali kila aliyempokea YESU KRISTO kama Mwokozi wake anauwezo wa kuomba kwa MUNGU Baba na kujibiwa.

2. Nchi ikatetemeka.
YESU KRISTO ndiye aliyeiumba Nchi yaani ardhi yote hivyo ardhi ilipata shinda sana kuupokea Mwili wa aliyeiumba.
Yohana 1:2-3 ''Huyo mwanzo alikuwako kwa MUNGU. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. ''
Pasipo YESU hakuna ambacho kingeumbwa, hivyo yeye ni muumbaji na aliumba hadi ardhi.
Ardhi ilitamani kukataa kuupokea Mwili wa YESU maana ardhi inajua hadhi ya Bwana YESU.
ardhi haikudhani kama hata siku moja mwili wa muumbaji ungeingia katika ardhi hivyo alidhi ilitetemeka sana na kuogopa maana ilijua YESU KRISTO ni nani.
Ardhi ni kama iliwaza ''Ni wapi tutamweka YESU?''
Maana hakukuwa na uwezekano wa YESU muumbaji wa ardhi kuingia ardhini.

3. Miamba ikapasuka.
Jambo la kwanza kujua katika hili ni kwamba YESU KRISTO ni Mwamba wa miamba yote.
1 Kor 10:4 ' wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni KRISTO. ''

Kwanini miamba ilipasuka?
Miamba ilipasuka kwa sababu ilikuwa inajisalimisha kwa Mwamba wa Miamba ambaye ni YESU KRISTO.
Miamba iliwakiliha watu wakubwa na mamlaka kuu, zote zilijisalimisha kwa Bwana YESU ndio maana hakuna mamlaka yeyote inayoweza kwenda kinyume na YESU ikafanikiwa.
Wateule wa MUNGU pia ni miaka ambayo iko chini ya Mwamba wa miamba ambayo ni YESU KRISTO.
Marko 16:18 ''Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. ''

Kumbuka pia kwamba YESU kama Mwamba hakika ukijenga nyumba yako juu mwamba uo hakika hakuna upepo wa kishetani au mvua za kichawi zitaiangusha nyumba yako.
Yaani ukimtegemea YESU na utakatifu hakuna anayeweza kukushinda aliye upande wa shetani.
Luka 6:48 ''Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.''
Hakika hakuna Mwamba kama MUNGU wetu ndio maana Miamba ilipasuka yaani ilijisalimisha kwake.
Isaya 44:8 '' Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko MUNGU zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine. ''
Hakika Miamba ilijisalimisha kwa Mwamba wa miamba maana Biblia inasema kwamba hakuna Mwamba kama JEHOVAH.
Kumbuka maana ya JEHOVAH ni MUNGU anayeokoa.
Na Sasa MUNGU anaokoa kupitia YESU KRISTO aliye mwamba wa milele.
Isaya 26:4 '' Mtumainini BWANA siku zote Maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.''
Hakika miamba ilikuwa na sababu za kujisalimisha kwa Mwamba wa milele.
Wateule wa MUNGU hatuogopi maana tunaye Mwamba wa milele.
Isaya 62:1-2 '' Nafsi yangu yamngoja MUNGU peke yake kwa kimya, Wokovu wangu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana ''

4. Makaburi yakafunuka na watakatifu wakafufuka na kuuenea mji.
Kuna siri kubwa juu ya hilo lakini kwa ufupi ni kwamba;
YESU KRISTO ana mamlaka yote hata aliweza kuwafufua watakatifu wote wa zamani na kuwahamishia mji mtakatifu.
Watakatifu sasa wala hawako kuzimu, wala hawako makaburini na wala hawako hewani bali wako mji mtakatifu.
Kila matakatifu wa KRISTO anapokufa duniani huenda mji mtakatifu ambao ni mbinguni na Bwana YESU ameshaandaa makazi huko ya watakatifu.
Yohana 14:1-3 ''1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. ''

Nyumbani mwa MUNGU kuna makao mengi, nyumbani mwa MUNGU ni mbinguni.
Ndio maana Bwana YESU alisema kwamba mteule wake akifa duniani anakuwa anaishi maana anakuwa yuko tayari mji mtakatifu.
Yohana 11:25-26 '' YESU akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? ''

Mtume Paulo kwa kulijua hilo alisema kwamba anatamni akaishi huko aliko KRISTO yaani mji takatifu ambapo ni mbinguni, Hata wateule wa KRISTO tunaoishi maisha matakatifu hakika tukiondoka duniani tutaenda mji mtakatifu.
Ona hii kiu ya Mtume Paulo ya kutaka kwenda kuishi mji mtakatifu.
Wafilipi 1:23 '' Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na KRISTO maana ni vizuri zaidi sana; ''

Kuna mambo mengi sana yalitokea baada ya Bwana YESU kufa na baadae kufufuka, nimekupa hayo manne yaliyo katika andiko moja tu lakini ukweli ni mambo mengi tu yaliyokea baada ya Bwana YESU kufa.
Nimalizie kwa kusema kwamba YESU KRISTO alikufa na kuzikwa na kisha akafufuka na sasa yu hai milele.
Mtume Yohana baada ya kumwona YESU akiwa katika utukufu wake baada ya kufufuka alianguka Yohana kwa hofu, Lakini Bwana YESU alijifunua kwa Yohana na kwako na kwangu kwamba yu hai milele na ana mamlaka yote.
Tumkimbilie tu yeye ili tuokoke.
Ufunuo 1:17-18 '' Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.''
MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

KAZI YA IMANI KATIKA MAOMBI.



1. Inakuondolea hofu, Woga na mashaka ndani yako.
2. Inakufanya umwamini MUNGU.
Waebrania 11:8-12

3. Inakupa kushinda
Mathayo 9:22

4. Inakupa kuwa mwenye haki.
Habakuki 2:4

5. Imani inakupa Ulinzi.
1 Petro 1:5

Nyongeza ni hii.
Katika Agano la kale Neno ''Imani'' Linapatikana katika maandiko mawili tu yaani Kumb 32:20 na Habakuki 2:4 lakini matukio ya kumwamini MUNGU ni mengi sana sana na hayo yanaonyesha Imani hata kama Hakuna Neno Imani.

Siku moja Nitalifafanua somo hili la KAZI ZA IMANI KATIKA MAOMBI.
MUNGU akubariki.

Kama MUNGU amekupa kufanya kazi yake hakikisha unaifanya kazi hiyo kwa moyo


Kama MUNGU amekupa kufanya kazi yake hakika inakupasa sana kuifanya kwa moyo na juhudi kubwa ili kuiepuka laana ya MUNGU. Kumbuka Biblia inasema amelaaniwa mtu yule aifanyaye kazi ya MUNGU kwa ulegevu.
kumbuka laana ni kitu kinachokukamata ili usiendelee.
Unaweza ukakataa kufanya kazi ya MUNGU kwa sababu tu wewe unataka kufanya biashara, lakini kila biashara utakayoifanya itakataa kwa sababu tu kuna laana ya kumgomea MUNGU kuifanya kazi yake. Dawa ni kutubu na kurudi kufanya maagizo ya MUNGU.

Ndugu, kama MUNGU amekupa kazi yake nakuomba Fanya kazi ya MUNGU kwa bidii na kwa moyo ili usiwe uliyelaaniwa.
Ubarikiwe

UZINZI NA UASHERATI MPAKA LINI?


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Kuna ndugu kaniambia kwanini sijapost neno la MUNGU leo, wakati najiandaa kuleta ujumbe ambao nilikuwa nimeukusudia MUNGU kanipa ujumbe huu, naomba kila ndugu asome hadi mwisho.Kama somo halifunguki hadi mwisho basi fungua koment litafunguka lote na hakika utabarikiwa kwa kujifunza.
Karibu.

Wanadamu Wengi Wanawake, Wanaume Na Vijana Wanatamani Kuacha Uasherati Lakini Hawawezi Kuacha. Unajua Ni Kwanini Hawataki Kuacha?
Ni Kwa Sababu Hawajaamua Kuacha, Maana Aliyeamua Kuacha Kitu Lazima Atakiacha Tu.
Biblia iko wazi kabisa juu ya kuwaonya wanadamu ili waache mabaya na kumpendeza MUNGU.

1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. ''
-Tumepewa agizo na amri kwamba tuukimbie uzinzi na uasherati.
-Kila mmoja anatakiwa kuacha uzinzi na uasherati.
-Kila mmoja anatakiwa asifurahie kuitwa kahaba au kuitwa malaya au kuitwa kiwembe au kuitwa basha bali kila mmoja atubu na kuacha dhambi hiyo mbaya.
unajua ni kwanini tunatakiwa kuikimbia zinaa?
Ni kwa sababu.
1Kor 6:16a ''Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? ''

-Ndugu kama hujui kwamba aliyeungwa na kahaba na yeye ameubeba ukahaba, basi tambua leo.
-Kama unatamani kuacha ukahaba lakini unaona kuna kitu kinakuzuia ni kwa sababu tu hujaamua kwenda mbinguni, ungeamua kwenda uzima wa milele ungeacha.
-Wengi wanafuga dhambi na kumpangia MUNGU siku yao ya kutubu. Kuna mtu anafanya maovu mengi tu lakini ukimwambia kwamba tubu na kugeuka anakuambia kwamba labda mwakani atatubu. Ukimuuliza kwamba ''je una uhakikka kwamba mwakani utakuwepo'' anasema ''labda tu'' kwahiyo kutubu ni labda na kuwa hai hiyo siku ya kutubu anasema ni labda tu. ndugu zangu hiyo ni hila ya shetani kuhakikisha kwamba wanadamu hawaendi uzima wa milele.
MUNGU anachukia sana uovu huu.
MUNGU hapa anasema '' Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba. Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake.-Yeremia 5:7-8 ''

-Ndugu, kama inakuhusu tubu leo na geuka, BWANA YESU yuko tayari kukusamehe kama ukiamua kumpokea na kutubu na kuanza kuishi maisha matakatifu.
- Kufuga Dhambi Ni Kujipeleka Jehanamu Mwenyewe. Unajua Kabisa Kwamba Unayoyafanya Ni Machukizo Kwa MUNGU Lakini Dhambi Hizo Unazifuga Mpaka Zimekua Na Umri Mkubwa Lakini Kutubu Hutaki. Siku Zote BWANA Anatuma Watumishi Wake Ili Tu Wewe Utubu Na Kumpokea YESU Lakini Wewe Umefanya Mgomo Baridi.BWANA anachukia uzinzi, ona hapa katika neno la unabii ambalo lina maana sana hata muda huu

Ezekieli 23:1-3,8,11,14,18 '' Nawezaje kukusamehe? Watoto wako wameniacha mimi, na kuapa kwa hao ambao si miungu; nilipokuwa nimewashibisha chakula, walizini, wakakutana wengi pamoja katika nyumba za makahaba. .....Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake. Wala hakuyaacha mambo yake ya kikahaba tangu siku za Misri, kwa maana wakati wa ujana wake walilala naye, wakayabana matiti ya ubikira wake wakamwaga uzinzi wao juu yake. ..... Na umbu lake, Oholiba, akayaona hayo walakini alizidi kuharibika kuliko yeye, kwa kupendelea kwake, na kwa uzinzi wake, uliokuwa mwingi kuliko uzinzi wa umbu lake. .... Naye akaongeza uzinzi wake; kwa maana aliona watu waume, ambao sura zao zimeandikwa ukutani, sura za Wakaldayo zilizoandikwa kwa rangi nyekundu; .... Basi alifunua uzinzi wake, na kufunua uchi wake; ndipo roho yangu ikafarakana naye, kama ilivyofarakana na umbu lake.''
-Ndugu kama inakuhusu basi tubu na kugeuka, uzinzi ni mbaya na wazinzi hawataurithi uzima wa milele labda watu kwanza.
-Umetenda sana dhambi hii, MUNGU amekuvumilia sana lakini leo anakuonya kupitia neno lake. Ndugu, Geuka, BWANA YESU atakusamehe na utaitwa mtakatifu badala ya jina lako lililozoeleka la kahaba au malaya.

Mathayo 5:27-30 '' Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. ''
-Ndugu, kama inakuhusu tubu na kugeuka.
-Kata mkono wako unaokukosesha yaani ailisha hata safari ya kwenda kuzini mliyoahidiana na yule ndugu.
-Ng'oa jicho lilaokukosesha yaani futa hata namba za huyo anayekulazimisha mwende kuzini, mshtaki hata kwa wazazi wako ili tu akome tabia yake hiyo mbaya.
Ndugu, Kufuga Dhambi Ni Kujipeleka Jehanamu Lakini Kutubu Na Kumpokea BWANA YESU Ni Kujipeleka Mbinguni. Wokovu Ni Kwa Ajili Yako Na Sio Wengine, Uzima Wa Milele Ni Kwa Ajili Yako Binafsi Na Sio Vinginevyo, Unaweza Ukaukosa Uzima Wa Milele Kama Tu Utaendelea Kufuga Dhambi Hadi Dhambi Hizo Zitazaa Jehanamu. BWANA YESU Anakuita Leo Ndugu Yangu, Mpokee Na Jina Lako Litaandikwa Kwenye Kitabu Chake Cha Uzima.

Marko 10:11-12 '' Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.''
-Ndugu, kama inakuhusu tubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea kama ukitubu na jina lako litabadilika, badala ya kuitwa mzinifu utaitwa mtakatifu. wafuate wachungaji wakusaidie.
Jiulize, Ukiwa Unaumwa Sana Kisha Ukaenda Hospital, Doctor Akakutibu Kisha Akakuambia Usile "Tena Chipsi Maana Zinazidisha Ugonjwa". Nakuambia Hata Kama Unazipenda Vipi Chipsi Lakini Hutakula, Hata Kama Ulikuwa Huwezi Kuishi Bila Kula Chipsi Wakati Huu Utaacha, Hata Kama Kuna Mtu Anakushawishi Utakataa, Utasema "Nikila Nitakufa" .
Sijui Kwanini Tunayatii Sana Ya Wanadamu Kuliko Ya MUNGU?. Ni Heri Tungemtii MUNGU Zaidi.
Wewe Mgonjwa(mwasherati) Mara Nyingi Umeenda Hospitali(kujifunza Neno La MUNGU), Daktari(BWANA YESU) Amekutibu(Umeombewa Na Kufunguliwa), Daktari Amekushauri Uache Kula Chipsi(uache Kuzini) Mbona Hutii?.

1 Kor 6:13-15 '' Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini MUNGU atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa BWANA, naye BWANA ni kwa mwili. Naye MUNGU alimfufua BWANA, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya KRISTO? Basi nivitwae viungo vya KRISTO na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! ''
-Ndugu mpendwa, kama inakuhusu tubu na kugeuka.
-Kama huwa unaenda kanisa ili kujificha tu wasikujue kwamba wewe ni mzinzi au mwasherati, tubu na kugeuka.
-Kama unatumika madhabahuni huku unafanya uzinzi au uasherati, tubu na kugeuka.
-Kama unaimba au huwa unahubiri harafu unauchafua mwili wa KRISTO, tubu na kugeuka.
BWANA YESU anakutaka ugeuke na kutubu leo.
Ndugu, Kama Umeamua Kabisa Kuacha Uzinzi Litii Neno La MUNGU. Kuna Hukumu Kwa Wazinzi.

Waebrania 13:4 '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.''
-Wewe kama ni mwanandoa lakini unaisaliti ndoa yako kila mara, tubu na kugeuka. kuna adhabu kwa wazinzi kama hawatatubu.
-Ndugu, kama inakuhusu, tubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea na jina lako litabadilika kutoka kuitwa mzinzi na kuwa mteule wa MUNGU.

2 Petro 2:14-15''wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana; wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;''
-Macho ya uzinzi?
ndugu tubu maana wewe kila binti akipita lazima umpigie mluzi maana una jicho la uzinzi.
-Ndugu tubu na kugeuka.
Najua inakuhusu ndio maana unatakiwa utubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea na utaanza kuitwa mtakatifu ukiwapigia mluzi wanadamu ili uwaambie kwamba '' Twendeni kanisani''

MUNGU Yuko Tayari Kumsamehe Yule Aliyeamua
1 Kor 6:9-11 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la BWANA YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu.''
Hakuna Mbingu Ya Wavaa Hirizi wala wazinzi, Tupa Hirizi Na na acha hirizi na Mpokee BWANA YESU Utaokoka.
Nimesema hivyo maana kuna watu hata huvaa hirizi ili kwa njia za kichawi wawapate vijana au mabinti na kufanya nao uzinzi.
Ndugu kama inakuhusu tubu na kugeuka, BWANA YESU atakupokea.

Ufunuo 18:3-6 '' kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na MUNGU amekumbuka maovu yake.Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.''
-Ana heri yule ambaye atabadilika baada ya kujifunza neno hili la MUNGU.
-Kikombe kimejaa na kilichobaki ni kutubu tu na kumpokea BWANA YESU.
Mwenye sikio la kusikia na asikie.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.