Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu namshukuru Mungu kutupa kibali katika siku ya leo kujifunza neno la uzima nakukaribisha sana.
Kila mwanadamu aliyechini ya jua anapaswa KUMTUMIKIA MUNGU kwa nguvu zake kwa akili,kwa Mali na muda pia.
Tambua usipo mtumikia Mungu utatumikia miungu au utatumikia upande mwingine usio na Mungu wa kweli.
KUMTUMIKIA MUNGU ni kusimama katika nafasi ya ufalme wa kimungu ili kulitumikia kusudi la Mungu na kumpendeza Mungu.Unaweza ukatumika katika karama,vipawa na huduma mbalimbali mfano uimbaji,utoaji,uinjilisti,ualimu,maombi na nafasi mbalimbali katika kristo Yesu.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UTUMISHI AU UNAPOMTUMIKIA MUNGU.
(1).Kuwa na muda mwingi wa kukaa uweponi mwa Mungu ukimsihi kuhusu utumishi wako.
Watu wengi hupenda KUMTUMIKIA Mungu lakini sio kukaa na Mungu hivyo mtu utamani Kuwa mwinjilisti,mchungaji au mwalimu mkubwa lakini sio maarufu ktk kutii na kumsikiliza Mungu
(2)Kumtafuta Mungu.Zaburi 105:4
Tumia muda mwingi Kumtafuta Mungu na sio kutafuta umaarufu Kama una huduma ya saa moja omba zaidi ya masaa sita jijengee tabia ya Kumtafuta Mungu mara kwa mara.Huku ukisoma neno kwa juhudi na kutamani kujua Siri za ufalme wa Mungu.
(3)Utukufu mpe Mungu pia tafuta Utukufu wa Mungu katika huduma yako.Zaburi 22:3. Wengi upenda majina yao yasifike na ya julikane ila sio Mungu wanaemtangaza ndio maana utakuta Mtumishi anasema kauli hi "watu wajue yupo fulani ktk mjii huu " Wala hasemi na ijulikane yupo Mungu Mwokozi mahali hapa.Wengi ujitwalia Utukufu kana kwamba wao utenda kwa nguvu zao.Mungu atusaidie.
(4)Tumika kwa bidii.Tia juhudi bila kukata tamaa Wala kufunjwa moyo usikate tamaa hata Kama watu hawawezi kukutia Moyo.Mathayo 11:13 na Luke 16:16.
(5)Mpende Mungu aliyekupa hiyo huduma.Wengi upenda huduma kuliko Mungu ndio maana mtu yupo tayari kutumika ktk Hali ya machukizo mbele za Mungu.Jitahidi usikosane na aliyekupa huduma ukawa bize na huduma kuliko aliyekupa huduma.Mathayo 22:37-38.Ishi katika maisha ya haki na utakatifu Yohana 15:14
(6)Toa zaka kwa uaminifu.Luka 11:42. Toa zaka iliyokamili mbele za Mungu usiwe mtu wa kumuibia Mungu ikawa dhambi kwako.Kuwa mwaminifu ili huduma yako ipate thawabu mbele za Mungu usiwe mtu mwenye hatia ktk utumishi wako.
Ubarikiwe Sana nakutakia utumishi wenye baraka
Ahsante.
Agnes Mwasambili
0769519697.
Saturday, October 12, 2019
Subscribe to:
Comments (Atom)
